Febuari 22, 2024 10:20
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

WAAGIZAJI WA PEMBEJEO WAONYWA KUFANYA UDANGANYIFU

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya uzalishaji, ubanguaji na masoko ya Korosho kwa msimu wa 2022/2023 kilichofanyika ukumbi wa PSSSF Jijini Dodoma, 24 April 2023, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Mohamed Bashe ametoa onyo kali kwa Wazabuni wa Pembejeo kuacha udanganyifu katika uagizaji wa pembejeo, onyo hili linalenga kuacha kufanya hujuma ambazo zinasababisha hasara kwa wakulima na wadau wa zao la Korosho.

Aidha, Mhe. Bashe amewaondoa hofu wakulima juu ya upatikanaji  wa pembejeo kwa msimu wa 2023/2024 na kusisitiza kwamba serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha kila mkulima aliyesajiliwa anapata pembejeo kwa wakati na zikiwa bora. Pia amewaomba wakulima kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba mara baada ya mauzo ya korosho ili kuweza kujinunulia pembejeo na kuhudumia mashamba yao bila kutegemea ruzuku ya Serikali muda  wote.

“Ruzuku iwe sehemu ya nyongeza kwa mkulima, lakini pia Serikali haijazuia Mkulima wa Korosho kununua pembejeo tu kama pembejeo hizo zimekaguliwa na kupitishwa na Mamlaka za Afya ya Mimea – TPHPA” Mhe.Hussein Bashe (MB)-DODOMA

Aidha, kupitia kikao hicho, Mhe. Bashe amepokea mapendekezo ya wajumbe ya namna bora ya uagizaji pemnbejeo kupitia kamati ya pamoja tofauti na njia ya uagizaji wa sasa na amesema atafanyia kazi mapendekezo hayo ili kuona kama itaweza kutatua changamoto zilizopo ili kuleta ufanisi upande wa Pembejeo.

Aidha, ameziagiza mamlaka zinazohusika na mimea na viuatilifu kuona namna ya kutafuta kinga kwa mimea na sio tiba ambazo kila mwaka zinajirudia hususani kwa zao la Korosho mbali na kuwa na hali ya hewa zinazo badilika kila msimu lakini magonjwa ni yaleyale.

Related posts

MKUU WA MKOA WA MTWARA AZINDUA MINADA YA KOROSHO KWA MSIMU WA 2022/2023 LEO TAREHE 21 OKTOBA KWA VYAMA VIKUU VIWILI TANECU NA MAMCU MKOANI MTWARA.

Peter Luambano

PEMBEJEO BILA MALIPO KWA WAKULIMA

Fesam

AUCTIONS TIME TABLE FOR THE SEASON 2022-2023

Peter Luambano