Febuari 13, 2025 09:49
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

NAIBU WAZIRI SILINDE AZINDUA MIRADI KATIKA SEKTA YA KILIMO

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amezindua Miradi itakayosaidia kuleta zaidi mageuzi katika Sekta ya Kilimo, inayofahamika kama SAGCOT: Support to SAGGOT Centre Ltd; na AGRA: Support to Tanzania’s Agriculture Transformation Office.

Dhumuni la miradi hiyo ni kupanua wigo wa maeneo ya Kilimo Tanzania, yaani “The Agriculture Growth Corridors of Tanzania (AGCOT) kufuatia kusainiwa kwa mkataba wa makubaliano kati ya Norway na AGRA.  Makubaliano hayo yamelenga kufungua vikwazo vya udhibiti wa kilimo ikiwa ni pamoja na vikwazo vya mauzo ya nje ili kuvutia uwekezaji wa Sekta Binafsi katika Sekta ya Kilimo nchini kupitia Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo (Agricultural Transformation Office – ATO).

Uzinduzi huo umefanyika tarehe 04 Februari 2025 jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tine Tonnes; Mtendaji Mkuu wa Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT), Bw. Geoffrey Kirenga; Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo (Agricultural Transformation Office- ATO), Bw. Jeremiah Temu; Mkurugenzi Mtendaji wa Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika, Prof. Jean Jacques Muhinda pamoja na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Kilimo na Mazingira.

Miradi yote itatekelezwa kwa miaka 3 (2025-2027) na itagharimu Dola za Marekani 1,348,466 sawa na shilingi 3,429,186,305 za Tanzania.

CHANZO: WIZARA YA KILIMO

Related posts

DKT SERERA AZINDUA MRADI WA GROWING TOGETHER

Amani Ngoleligwe

BODI YA KOROSHO TANZANIA YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI WA KILIMO MHESHIMIWA HUSSEIN BASHE (MB)

Peter Luambano

SEKTA YA KILIMO KUZIDI KUIMARIKA

Amani Ngoleligwe