Aprili 22, 2024 01:17
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

KOROSHO QUEENS YAPATA UFADHILI WA VIFAA VYA MICHEZO

Bodi ya korosho imekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo Mipira,Viatu na Sare kwa timu ya mpira ya KOROSHO QUEENS siku ya tarehe 11/05/2023 katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Korosho Mtwara,makabidhiano hayo yamefanywa kati ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi Ndug. Gerald Rogathe na uongozi wa KOROSHO QUEENS wakiongozwa na Meneja wa Timu hiyo Ndug. Hussein Omary Kibombwe.

Vifaa hivyo vimetolewa na Bodi ya korosho kwa kuzingatia ombi la ufadhili lililoletwa na KOROSHO QUEENS,aidha kwa kuzingatia umuhimu wa michezo,Bodi imetekeleza ombi hilo kama walivyoleta na pia imewaomba wadau wengine wa michezo kuchangia na kutoa chochote ili kuendeleza ndoto ya timu hii iliyopo mjini Mtwara.

Related posts

TBS Yatoa Mafunzo Ya ISO9001 Bodi Ya Korosho Tanzania

Fesam

Kikao cha ufunguzi wa zoezi la ukaguzi wa hesabu za taasisi Kwa mwaka 2021/2022

Peter Luambano

WAAGIZAJI WA PEMBEJEO WAONYWA KUFANYA UDANGANYIFU

Peter Luambano