Novemba 9, 2024 06:23
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

KOROSHO MARATHON YAFIKA KILELENI KWA SHANGWE

Mbio za Korosho Marathon ambazo zimeongozwa na naibu waziri wa utamaduni sanaa na michezo Mhe. Hamis Mwinjuma hatimaye zimefika kileleni kwa shangwe kubwa huku washindi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wakipata zawadi zao.

Hii ni awamu ya tatu ya mbio hizi ambazo kwa mwaka huu kilele chake kilikuwa katika viwanja vya Milleneum beach mkoani Mtwara oktoba 26, 2024 ambapo mgeni rasmi mheshimiwa naibu waziri Hamis Mwinjuma ameipongeza bodi ya korosho kwa usimamizi wake mzuri.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya Korosho Tanzania ndg. Francis Alfred amemshukuru Mhe. Naibu Waziri kwa ushiriki wake na kuahidi kuendelea kufanya vema zaidi katika nyakati zijazo kwani Korosho Marathon imekuwa na msaada mkubwa kwa jamii nzima.

Hata hivyo ndg. Alfred alipokuwa akieleza juu ya kazi zinazofanywa na Bodi ya Korosho Tanzania amemshukuru Rais dkt. Samia Suluhu Hassan kwa pembejeo za ruzuku kwani ni Dhahiri kuwa zimeongeza uzalishaji katika msimu huu na hivyo wakulima kupata kipato kikubwa kupitia korosho zao.

Kilele cha Korosho Marathon kwa mwaka huu kilikuwa ni tarehe 26 oktoba 2024 na hii ikiwa ni awamu ya tatu ya Korosho Marathon, ambapo kwa mara ya kwanza ilizinduliwa mwaka 2022 ikiwa na watu wapatao 450 waliojisajili, mwaka 2023 waliojisajili walikuwa 1763 na mwaka huu waliojisajili ni zaidi ya watu elfu moja.

Related posts

NYONGEZA NA. 1 YA MWONGOZO NA. 2 WA USIMAMIZI NA UDHIBITI UBORA WA KOROSHO GHAFI KWA MWAKA 2023/2024

Peter Luambano

MAONESHO YA NANENANE 2022-MBEYA

Fesam

TARI WAJIANDAA KUPOKEA MEDALI KOROSHO MARATHON

Amani Ngoleligwe