Januari 16, 2026 05:29
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

DKT. KIRUSWA ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO CBT NA KUPONGEZA JUHUDI ZA RAIS DKT. SAMIA

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wakulima wa korosho ikiwa ni pamoja na kuwapatia pembejeo za ruzuku na kuwa na utashi wa kisiasa katika kuendeleza Sekta ya Kilimo nchini.

Pia Dkt. Kiruswa ameipongeza Bodi ya Korosho Tanzania kwa kazi nzuri wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kuwasimamia wakulima wa zao la korosho wa Kanda ya kusini na mikoa mingine nchini.

Ameyasema hayo leo juni 13, 2024 alipotembelea banda la Bodi ya Korosho wakati wa Maonesho ya Madini na Uwekezaji wilayani Ruangwa mkoani Lindi. Maonesho hayo yameanza rasmi tarehe 11 na yanatarajiwa kufikia tamati tarehe 14 juni 2025.

Related posts

FURSA ZA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA

Peter Luambano

VIONGOZI CBT WAKUTANA NA WAGENI KUTOKA UHOLANZI KUJADILI UONGEZAJI THAMANI ZAO LA KOROSHO

Amani Ngoleligwe

MATUMINZI YA SERIKALI MTANDAO KATIKA UTUNZAJI NYARAKA

Peter Luambano