
Bodi ya korosho Tanzania ni Taasisi ya Umma iliyoko chini ya Wizara ya Kilimo iliyoundwa chini ya sheria ya Tasnia ya korosho Namba 18 ya mwaka 2009 (sura ya 203 ya sheria ya Tanzania) na kanuni zake za mwaka 2010 inayoipa jukumu la usimamizi wa Tasnia ya korosho kwenye mnyororo mzima kuanzia kwa mkulima hadi kwa mlaji wa mwisho.
Maono
Kuwa taasisi shindani, mahiri na endelevu katika usimamizi wa Tasnia ya korosho.
Dhima
Kuendeleza,kusimamia na kudhibiti masuala yote yanayohusiana na Tasnia ya korosho kwa ufanisi na kwa kutenda haki.
This is custom heading element
Maadili na Msingi
1.Kumjali mteja
2.Uadilifu katika utoaji huduma
3.Kutokuwa na upendeleo wa aina yoyote
4.Uwajibikaji wa hali ya juu
5.Kutoa huduma kwa uwazi