Novemba 28, 2023 06:41
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UGAWAJI WA PEMBEJEO KWA MSIMU WA 2023/2024


Timu ya watalaam wa TEHAMA kutoka BIZY TECH kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho ikiongozwa na mjumbe wa kamati ya Pembejeo Ndug. Andambike Mwakilema imefanya ziara ya ukaguzi wa baadhi ya pembejeo ambazo tayari zimeshawasili Nchini katika moja ya Ghala la kuhifadhia ikiwa ni maandalizi ya utekelezaji wa Agenda ya 10/30 ya Wizara ya Kilimo.
Lengo la ukaguzi huu ni kukamilisha zoezi la uwekaji alama za kielektroniki (QR CODES) kwenye kila kifungashio cha pembejeo ikiwa ni hatua ambayo serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassani ya utekelezaji wa matumizi ya Teknolojia katika utendaji wa Serikali ili kuongeza uwazi na uwajibikaji.
Bodi ya Korosho ipo katika zoezi endelevu la usajili wa wakulima wa Korosho kwa njia ya kielektroniki Nchi nzima,lengo mahususi ni kuiwezesha Sekta ya Kilimo kuwa na kanzi data ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya Kilimo, na kwa hatua hii,msimu wa 2023/2024, kila pembejeo itatolewa kwa njia ya kielektroniki kwa wakulima wote waliosajiliwa na hivyo kurahisha ufuatiliaji na upatikanaji wa takwimu kwa urahisi.

Related posts

MAPOKEZI YA VIWATILIFU MKOANI MTWARA

Fesam

PEMBEJEO BILA MALIPO KWA WAKULIMA

Fesam

Bodi Ya Wakurugenzi Ya Bodi Ya Korosho Imefanya Vikao Vyake Toka 29.10.2021 Na 30.10.2021

Fesam