Julai 17, 2025 08:15
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

SILINDE ASHIRIKI COP29 NCHINI AZERBAIJAN.

Mhe.David Silinde (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo akiambatana na Dkt. Hussein Omary, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo (Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula) pamoja na wataalam wengine wa Wizara ya Kilimo wameshiriki katika Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unaofanyika katika mji wa Baku, nchini Azerbaijan.

Katika Mkutano huo, Wizara imeshiriki katika majadiliano na Mwakilishi wa Mfuko wa Ufadhili wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund) na kujadili masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na namna ya kuwasilisha miradi ya vipaumbele ya pamoja kwa mfuko huo kwa mwaka 2025.

CHANZO: Wizara ya Kilimo

Related posts

RULES AND SALES CONDITIONS FOR THE 2023/2024 CROP SEASON

Peter Luambano

WAKULIMA MNOLELA: TANGU TUANZE KUPOKEA PEMBEJEO ZA RUZUKU MAMBO YANAKWENDA VIZURI SANA

Amani Ngoleligwe

UGAWAJI WA PIKIPIKI KWA MAAFISA UGANI-LINDI

Peter Luambano