Julai 12, 2025 11:43
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

WAKULIMA TANECU WAUZA KOROSHO ZAO KATIKA MNADA WA SITA

Wakulima wa zao la korosho kutoka Chama Kikuu Cha Ushirika TANECU katika mnada wake wa sita uliofanyika Nov 15 2024, wilayani Tandahimba mkoani Mtwara wameuza korosho zao kwa Bei ya juu ya Tsh.3240/= na ya chini ikiwa Tsh.3010=

Jumla ya Tani 17233,875 za korosho ghafi kati 18966,934 zimeuzwa, na zilizobaki ni Tani 1733 ambazo zitauzwa katika mnada wa sita wa Chama Kikuu Cha Ushirika Lindi Mwambao hapo Nov 16-2024.

Mnada huo umefanyika kupitia mfumo wa soko la bidhaa Tanzania (TMX) ukihudhuriwa na maafisa kutoka Bodi ya Korosho Tanzania, viongozi wa TANECU, na wakulima wa korosho kutoka wilaya za Newala na Tandahimba.

Related posts

KABRASHA KIKAO CHA TATHMINI 2025

Amani Ngoleligwe

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano wa kimataifa wa korosho uliofanyika Tanzania katika ukumbi wa Mikutano ya kimataifa wa Julius Nyerere

Peter Luambano

BEI YA JUU YA KOROSHO YALETA SHANGWE KWA WAKULIMA KATIKA MNADA WA KWANZA MKOANI MTWARA

Amani Ngoleligwe