Machi 26, 2025 07:02
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

MKURUGENZI MKUU CBT: KOROSHO MARATHON HUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII, HUTOA FURSA ZA AJIRA

Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania ndg. Francis Alfred oktoba 24, 2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Bodi ya Korosho Mtwara-Tanzania, katika kuelekea Korosho Marathon ametaja mambo muhimu ambayo Bodi ya Korosho inayafanya kupitia Korosho Marathon kuwa ni pamoja na kuelezea fursa zote za zao la korosho kuanzia shambani, ubanguaji, usindikaji na masoko.

Pia amesema kuwa Bodi ya Korosho kupitia Korosho Marathon inatengeneza uelewa wa mchango wa zao la Korosho katika kuinua uchumi wa mikoa ya kusini mwa Tanzania kwa maana ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ikiwa ni Pamoja na upatikanaji wa ajira kwa wanawake na vijana.

Ameongeza kuwa washiriki wate watakaofika katika korosho Marathon mwaka huu watapata furasa za kutembelea vivutio vya utalii kwani Korosho Marathon pia ni Daraja katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika mikoa ya kusini ambapo wadau kutoka ndani na nje ya nchi huja kujifunza juu ya mambo ya kale na mambo yanayofanyika sasa.

Kwa upande wake mratibu wa Korosho Marathon mwaka huu wa 2024 anayeshirikiana na Bodi ya Korosho ndg. Nelson Mrashan amesema kuwa hadi sasa ni zaidi ya washiriki elfu moja wameweza kujisajili ili kushiriki mashindano hayo.

Pia ndg. Mrashan ameishukuru Bodi ya Korosho Tanzania kwa kumuamini na kumpa ushirikiano ikiwa ni Pamoja na kumuwezesha kwa namna mbalimbali ili kuratibu vema mashindano hayo.

Kilele cha Korosho Marathon kwa mwaka huu ni tarehe 26 oktoba 2024  na hii ikiwa ni awamu ya tatu ya Korosho Marathon, ambapo kwa mara ya kwanza ilizinduliwa mwaka 2022 ikiwa na watu wapatao 450 waliojisajili na mwaka 2023 waliojisajili walikuwa 1763.

Related posts

RATIBA YA MINADA KWA MSIMU WA 2023/2024

Peter Luambano

MAAFISA KILIMO WA BBT KOROSHO WAENDELEA NA MAFUNZO YA VITENDO

Amani Ngoleligwe

MKUU WA MKOA WA MTWARA KANALI AHMED ABBAS AHMED AZINDUA RASMI KOROSHO MARATHON MSIMU WA PILI 2023

Peter Luambano