Disemba 11, 2024 10:42
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

DKT. SERERA AONGOZA KIKAO NOVEMBA 13-2024

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo (Ushirika na Umwagiliaji), Dkt. Suleiman Serera ameongoza kikao cha pamoja kati ya Wizara na Washiriki wa Maendeleo tarehe 13 Novemba 2024 kujadili namna Wizara inavyotekeleza majukumu yake yanayohusu usalama wa chakula, mfumo wa usajili wa wakulima pamoja na kilimo kinachokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi (Climate Smart Agriculture) kwa ajili ya maoni yatakayotumika katika kuandaa Mpango wa Awamu ya Tatu wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN III) utakaotekelezwa na TASAF.

Timu hiyo imehusisha wataalamu mbalimbali kutoka Benki ya Dunia, Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Uswizi, Ubalozi wa Uingereza, Irish Aid, Jumuiya ya Madola, Umoja wa Ulaya, WFP na UNISEF wakiongozwa na Claudia Zambra kutoka Benki ya Dunia.

CHANZO: Wizara ya Kilimo

Related posts

TICC-WAJUMBE WAKIWA KWENYE MKUTANO JNICC DAR ES SALAAM

Peter Luambano

MAFUNZO YA UHUISHAJI NA USAJILI WA WAKULIMA WA KOROSHO

Peter Luambano

MKURUGENZI MKUU CBT: KOROSHO MARATHON HUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII, HUTOA FURSA ZA AJIRA

Amani Ngoleligwe