Wakati minada ya korosho katika msimu wa 2024/2025 ikiendelea, Mkurugezi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndg. Francis Alfred alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari novemba 4, 2024 amesema kuwa jumla ya Tsh bilioni 743.57/= zimepatikana Katika wiki nne za minada ya korosho.
Huku wakulima zaidi ya asilimia 90 wakiwa wamelipwa fedha zao hadi sasa, bei za korosho katika minada inayoendelea ni nzuri na sababu kubwa zikitajwa kuwa ni usimamizi mzuri wa Vyama Vikuu vya Ushirika, Bodi ya Korosho Tanzania na ubora wa korosho zinazouzwa.
Changamoto mbalimbali ikiwamo ya usafiri na malipo zimeendelea kushughulikiwa kwa ukaribu ambapo magari yameongezwa ili kubeba korosho kutoka vyama vya msingi kuelekea ghala kuu na wakulimwa wenye changamoto ya malipo wamekumbushwa kuwasiliana na viongozi wa AMCOS au Bodi ya Korosho Tanzania kwa utatuzi zaidi.
“Tayari tumeongea na Vyama vya Ushirika kuhakikisha wanafuatilia hizo changamoto ndogo ndogo na kwenda kwenye benki husika ili akaunti zote ambazo zina changamoto wakulima wapatiwe stahiki zao.” Ndg. Alfred
Vilevile Mkurugenzi mkuu amewatoa wasiwasi wakulima kuwa zoezi hilo litalishugulikiwa ndani ya wiki hii na malipo yote yaliyo kwama Katika minada iliyopita, viongozi watahakikisha wakulima wanapatiwa haraka iwezekanavyo.