Aprili 20, 2025 12:38
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

KATIBU MKUU MWELI AKUTANA NA BALOZI WA ITALIA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Giuseppe Sean Coppola jijini Dodoma tarehe 5 Novemba 2024.

Viongozi hao wamekutana kwa ajili ya utambulisho na kuzungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano katika Sekta ya Kilimo hususan katika masuala ya utafiti ili kuchochea ugunduzi wa teknolojia mbalimbali kwenye Sekta hiyo.

Mhe. Balozi Coppola ameelezea kuwa Italia ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha mnyororo wa thamani wa zao la kahawa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Mweli alimshukuru Mhe. Balozi Coppola na kueleza kuwa Wizara ya Kilimo ina fursa za uwekezaji hivyo alihamasisha na kukaribisha wawekezaji kutoka nchini Italia kuwekeza katika Sekta ya Kilimo nchini; hususan katika maeneo ya uzalishaji wa zana za kilimo kama vile matrekta.

CHANZO: Wizara ya Kilimo

Related posts

Bodi Ya Wakurugenzi Ya Bodi Ya Korosho Imefanya Vikao Vyake Toka 29.10.2021 Na 30.10.2021

Fesam

RULES AND SALES CONDITIONS FOR THE 2023/2024 CROP SEASON

Peter Luambano

TANGAZO KWA WADAU WOTE WA TASNIA YA KOROSHO NCHINI. NOV 11-2024

Amani Ngoleligwe