Dk. Hussein M. Omar, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo ameshiriki katika kikao kazi kati ya Tanzania na Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Bavaria, nchini Ujerumani. Ujumbe wa wafanyabiashara hao uliongozwa na Mhe. Tobias Gotthardt Naibu Waziri wa Uchumi, Maendeleo ya Kikanda na Nishati wa Jimbo la Bavaria, Ujerumani.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 01 Novemba, 2024 katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo Jijini Dar es Salaam ambapo kilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mhe. Hassan Iddi Mwamweta, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani pamoja na Viongozi na Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine Viongozi hao walijadiliana kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Bavaria. Wakati wa majadiliano, Dk. Hussein alieleeza kuhusiana jitihada mbalimbali zinazofanyika na Serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha Sekta ya Kilimo ikiwemo, kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali, kuimarisha miundombimu ya umwagiliaji, kuongeza upatikanaji wa pembejeo za kilimo na Sekta ta Kilimo inavyochangia katika upatiakanaji wa ajira kwa vijana kupitia Programu ya Jenga Kesho Bora (BBT-YIA).
Aidha, alieleza kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Bavaria katika maeneo mbalimbali ya ambaoo alieleza kuwa, Tanzania na Bavaria zinaweza kushirikiana katika kuimairisha utafiti katika kilimo kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa mbegu bora zinazostahmili ukame, teknolojia za uzalishaji wa mazao mbalimbali, kushirikiana katika katika kuongeza upatkanaji wa masoko ya mazao na eneo la uongezaji thamani wa mazao na teknolojia za kuhifadhi mazao ya wakulima.
Kwa upande Mhe. Tobias Gotthardt alieleza kuwa Serikali ya Ujerumani iko tayari kushirikiana na Tanzania kwa kubadilishana teknolojia za kisasa na mifumo bora ya Kilimo wanayotumia wananchi wa Bavaria, itayowezesha wakulima wa Tanzania kuinua kiwango cha uzalishaji mazao mbalimbali ili iweze kuzalisha mazao hayo na yaweze kupata soko katika Bara la Ulaya.