Machi 26, 2025 07:29
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

RAIS DKT SAMIA ASHIRIKI MIKUTANO MUHIMU KUHUSU KILIMO-MAREKANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki katika mijadala muhimu ya kimataifa kuhusu kilimo barani Afrika ambayo ni Africa Agriculture Dialogue (AAD) ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB); na mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug, ulioandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation katika mji wa Des Moines, jimbo la Iowa, Marekani, mnamo Oktoba 30, 2024.

Katika hotuba zake, Mhe. Rais Dkt. Samia ameeleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Tanzania ili kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula kwa ajili ya kujitosheleza kama Taifa na kuuza Chakula cha ziada kibiashara (feed ourselves, feed others commercially). Aidha, Mhe. Rais Dkt. Samia alibainisha jinsi nchi inavyoimarisha mifumo ya uzalishaji wa chakula kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kufikia malengo hayo kama Taifa.


Mikutano hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb); Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Zanzibar, Mhe. Shamata Shaame Khamis (Mb); na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli.

Related posts

TANI 180,342 ZA KOROSHO ZAUZWA NDANI YA WIKI TATU MSIMU WA 2024/2025.

Amani Ngoleligwe

HALI YA SOKO LA KOROSHO GHAFI KWA MWAKA 2022/2023

Peter Luambano

NYONGEZA NA. 1 YA MWONGOZO NA. 2 WA USIMAMIZI NA UDHIBITI UBORA WA KOROSHO GHAFI KWA MWAKA 2023/2024

Peter Luambano