Mafunzo hayo yanalenga kuelekeza matumizi sahihi na salama ya viuatilifu wilayani Biharamulo sambamba na kuwapatia pembejeo za kudhibiti magonjwa na wadudu waharibifu kwenye zao la korosho. Mafunzo hayo yamepangwa kutolewa kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 28 Oktoba 2022 kufuatia kubainika kuwepo kwa wakulima wa korosho wilayani humo ambapo Bodi ya korosho inatarajia pia kuwajengea uwezo wa kubangua korosho wakati bado wanaendelea kuongeza uzalishaji wa zao ilo.