Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi la Bodi ya Korosho Ndg.Francis Alfred ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania akiongoza kikao cha mwisho wa mwaka cha baraza la wafanyakazi leo tarehe 16 Desemba, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya korosho Mtwara.
Baraza hilo linalojumuisha wajumbe mbalimbali wakiwemo wakuu wa Idara na Vitengo,Mameneja wa matawi na wajumbe wa kuchaguliwa,lengo la kikao hiki ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uendelezaji wa Tasnia ikiwa ni Pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu ustawi wa wafanyakazi.