Mei 29, 2024 02:17
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

Kikao cha 12 cha Bodi ya Wakurugenzi

Bodi ya Wakurugenzi katika kikao chake cha robo ya tatu ya mwaka 2023/2024 ili kupitia na kujadili taarifa ya utekelezaji iliyowasilishwa na Menejimenti imetoa maelekezo mahsusi ikiwemo usimamizi wa mradi wa ujenzi wa Kongani la Viwanda vya kubangua korosho kijiji cha Maranje Mkoa wa Mtwara.

Bodi imeelekeza menejimenti kusimamia mradi huu kwa weledi mkubwa ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lengo ni kuhakikisha kuwa korosho zinabanguliwa ndani ya nchi na siyo kuuza korosho ghafi nje.

Aidha, Bodi imesisitiza menejimenti kusimamia shughuli za uendelezaji zao la korosho hasa kipindi hiki cha mvua ili kuongeza uzalishaji kutoka tani 305,000 za sasa hadi kufikia tani 595,000 msimu wa 2024/2025 kwa kuwa ndiyo malengo ya uzalishaji.

Akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Brg. Gen. Mstaafu Aloise Mwanjile ndc amesisitiza menejimenti kutekeleza maazimio ya kikao cha tathmini ya uzalishaji, ubanguaji na masoko ya korosho kwa mwaka 2023/2024 na mipango ya mwaka 2024/2025.

Related posts

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano wa kimataifa wa korosho uliofanyika Tanzania katika ukumbi wa Mikutano ya kimataifa wa Julius Nyerere

Peter Luambano

TANGAZO LA KAZI

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO YAPOKEA TANI 3,680 YA SULPHUR KUPITIA BANDARI YA MTWARA

Peter Luambano