Julai 27, 2024 08:17
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

MATUMINZI YA SERIKALI MTANDAO KATIKA UTUNZAJI NYARAKA

Ndg.Joseph M Ndaro pamoja na Ally Ally kutoka Idara ya kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wametoa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kielektroniki Bodi ya korosho Tanzania; wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Ndg.Francis Alfred,watumishi wote kwa ngazi zote za kiutawala wamefurahia mafunzo hayo ili kurahisisha utendaji kazi wa kila siku.

Faida ya matumizi ya mfumo huu ni pamoja na kuongeza ufanisi katika utunzaji na usambaza nyaraka za wateja na ofisi,hii itasaidia kupunguza malalamiko ya ucheleweshwaji wa huduma kwa wateja lakini pia upotevu wa nyakara aidha kwa makusudi au bahati mbaya.

Kwa hatua hii,Bodi ya Korosho itaondokana na changamoto za mteja kutotendewa haki katika kuhudumiwa na kucheleweshwa kuhudumiwa kwa wakati “Tunapenda kuutarifu umma kwa ujumla kwamba sasa tunaingia kwenye matumizi ya elektroniki kwa kupokea nyaraka zote kuanzia ofisi ya kumbukumbu (masijala),kusambazaji ndani ya ofisi kwa Idara zote ili kuongeza thamani ya matumizi ya muda katika kutoa huduma kwa wateja wetu sambamba na huduma ya nyaraka kwa watumishi ndani ya Ofisi na Taasisi zingine zilizopo kwenye mfumo huu”Francis Alfred (Makao Makuu ya Bodi ya Korosho Mtwara).

Related posts

MWONGOZO WA SOKO LA AWALI KWA MSIMU WA 2023/2024

Peter Luambano

KOROSHO QUEENS YAPATA UFADHILI WA VIFAA VYA MICHEZO

Peter Luambano

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano wa kimataifa wa korosho uliofanyika Tanzania katika ukumbi wa Mikutano ya kimataifa wa Julius Nyerere

Peter Luambano