Elimu ya kujikinga na kupambana na virusi vya ukimwi (HIV) kazini yakitolewa na Dr Mbelenje katika ukumbi wa Bandari Mtwara tarehe 15 desemba, 2022 kutoka Wizara ya Afya kwa watumishi wa Bodi ya korosho Nchini,Bodi ya korosho imekua na utaratibu wa kualika wataalam mbalimbali katika sekta tofauti kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa watumishi wake
Katika utamaduni huo,Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya korosho Tanzania imejiwekea utaratibu wa kufanya mafunzo na Elimu juu ya masuala mbalimbali ikiwemo Afya kila mwaka kwa watumishi wake,lengo kuu ni kuwajengea uwezo na uelewa ili wawe na Afya njema ambayo itawafanya wawezi kufanya kazi kwa ustadi na maarifa katika kukuza uchumi wao na Nchi kwa ujumla.