Mei 4, 2024 06:48
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

KIKAO CHA TATHMINI YA UZALISHAJI, MASOKO NA UBANGUAJI WA KOROSHO MSIMU WA 2023/2024

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) ameongoza Mkutano wa Tathmini ya Uzalishaji, Ubanguaji na Masoko ya zao la Korosho kwa msimu wa Mwaka 2023/2024 na kujipanga kwa msimu wa Mwaka 2024/2025 katika Ukumbi wa PSSSF, jijini Dodoma tarehe 22 Aprili 2024.

“Lazima tubadilike na tubadilishe maeneo ya kimfumo ili kuzidi kuongeza tija kwenye zao la Korosho. Tuongeze maafisa ugani, mbegu na dawa bora kukabiliana na ugonjwa wa blaiti; pamoja na kununua excavator, bulldozer, na kuchimba mabwawa madogo kwa ajili ya mahitaji kwa Wakulima,” amesema Waziri Bashe.

Amepokea pia taarifa ya Kamati maalum ya uchambuzi wa Tasnia ya Korosho iliyoongozwa na Mwenyekiti Chacha na kuelekeza kuwa Watumishi waliobainika kwa ubadhirifu wa mali za Umma watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu-Kazi Maalum, George Mkuchika, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho, Bw. Francis Alfred, Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho, Brig. Gen. (mstaafu) Aloyce D. Mwanjile, ndc; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo; Waheshimiwa Wabunge kutoka Mikoa inayolima korosho, wakulima, wafanyabiashara na wadau wengine.

Related posts

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KWA WAKULIMA WA KOROSHO

Peter Luambano

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano wa kimataifa wa korosho uliofanyika Tanzania katika ukumbi wa Mikutano ya kimataifa wa Julius Nyerere

Peter Luambano

TANGAZO LA KAZI

Peter Luambano