Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji , wameitembelea Bodi ya Korosho Tanzania kwa ajili ya kujifunza shughuli mbali mbali zinazofanywa ikiwa Pamoja na Masuala ya Pembejeo, Kilimo , Ubanguaji na Masoko.
Katika ziara hiyo Baraza la Madiwani waliweza kupata taarifa mbalimbali zinzohusu zao la Korosho Pamoja na kujifunza namna bora ya kuongeza thamani katika zao hilo, hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Bwana Francis Alfred aliwaomba Waheshimiwa Madiwani kuwa Bodi imeomba eneo katika wilaya yao ya Rufiji jumla ya Hekali 5,000 ambapo ndani ya hekali hizo kutakuwa na Mashamba Makubwa ya Pamoja kwa ajili ya Vijana wa Rufiji, Wafanyakazi wa Bodi ya Korosho Tanzania na Makatibu Wakuu wa Wizara zote, hivyo iwapo Bodi itapatiwa eneo hilo basi Rufiji itakuwa ni moja ya sehemu yenye mashamba makubwa ya mfano Tanzania.