Disemba 11, 2024 09:48
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BODI YA KOROSHO YAPOKEA TANI 3,680 YA SULPHUR KUPITIA BANDARI YA MTWARA

Serikali kupitia Bodi ya Korosho imeendelea na jitihada za kumkwamua mkulima wa Korosho ili kuongeza tija na uzalishaji kufikia agenda ya 10/30 ifikapo 2030. Mkakati wa utoaji wa ruzuku ya pembejeo ambayo utaenda kumsaidia mkulima ili aweze kunufaika na zao lake.
Mpaka kufikia tarehe 25 Mei, 2023, zaidi ya tani 10,000 za Sulphur ya Unga imepokelewa ili kufikia lengo la tani 49,000 ambayo itafanya kuwa na ziada ya Sulphur kwa msimu ujao.
Akiongea katika mapokezi ya Sulphur tani 3,680 ikiwa ni sehemu ya tani 10,000 zilizopokelewa msimu wa 2023/2024, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameipongeza Bodi ya Korosho kwa kufanikisha malengo ya serikali na kwa jitihada kubwa inayofanya ili kuhakikisha zao la Korosho linamnufaisha mkulima.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Ndug.Francis Alfred ameishukuru serikali kwa jitihada zake hususani katika kumsaidia mkulima wa Korosho nchini, ameongeza kuwa mpaka sasa kiasi kikubwa cha pembejeo kimewasili. Viuatilifu vya maji Lita 1,300,000; Sulpur ya unga tani 10,189 na Mabomba 5,000 ya kupulizia ambayo ni zaidi ya mahitaji ya sasa.
Amewasihi wakulima kuendelea kujisajili kwenye kanzidata ya wakulima ili kuisadia serikali kuweka malengo sahihi ya kuendeleza zao.

Related posts

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano wa kimataifa wa korosho uliofanyika Tanzania katika ukumbi wa Mikutano ya kimataifa wa Julius Nyerere

Peter Luambano

MWONGOZO WA SOKO LA AWALI KWA MSIMU WA 2023/2024

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO TANZANIA YAENDELEA NA UBORESHAJI WA KANZI DATA YA WAKULIMA

Peter Luambano