Septemba 12, 2024 10:32
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

MAFUNZO YA UHUISHAJI NA USAJILI WA WAKULIMA WA KOROSHO

Bodi ya korosho Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya serikali za Mtaa imefanya mafunzo ya matumizi ya vifaa vya kielektroniki  tarehe 10 Januari 2023 kwaajili ya uhuishaji na usajili wa kanzidata ya wakulima wa korosho kwa awamu ya kwanza katika Halmashauri mbili za Mkoa wa Mtwara.

Mafunzo haya yametolewa kwa Maafisa watendaji wa Vijiji,Kata na Maafisa Ugani kutoka kila kijiji ndani ya Halmashauri husika,kwa awamu ya kwanza ambapo zoezi hili litadumu kwa siku kumi na nne katika Wilaya ya Mtwara yenye Halmashauri mbili;Mtwra Mjini na Vijijini.

Zaidi ya washirki 250 wamepatiwa mafunzo haya na kukabidhiwa vifaa tayari kwa kuanza zoezi la uhuishaji tarifa rasmi,aidha zoezi hili linatarajia kuchukua takribani miezi mitatu lakini pia litakua endelevu kila baada ya muda maalumu ili kuifanya kanzidata ya wakulima wakorosho kuwa hai na yenye tarifa sahihi.

Akizungumza katika mafunzo hayo,mgeni rasmi,Mkurugenzi kwa kituo cha utafiti wa kilimo(TARI)-Naliendele Dkt.Fortunus Kapinga,amewaasa washirki kuzingatia waliyofundishwa na kuwa wazalendo ili kufanikisha zoezi hili kwa pamoja na kufikia lengo la Serikali la uzalishaji wa korosho Nchini.

Related posts

SALES CATALOGUE -TANECU TANDAHIMBA

Peter Luambano

Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango amefungua Mkutano wa Kimataifa wa Korosho wa siku tatu hapa nchini

Peter Luambano

ELIMU YA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA UKIMWI KWA WAFANYAKZI WA BODI YA KOROSHO

Peter Luambano