Disemba 11, 2024 10:11
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

WAKULIMA WAISHUKURU SERIKALI MFUMO WA TMX

Baadhi ya wakulima wa zao la Korosho wilayani Newala mkoani Mtwara wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utaratibu mzuri wa kuuza zao la korosho kupitia mfumo wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), mfumo ambao husimamia mnada kijiditali kwa lengo la kuwaongezea uhakika wa masoko, uhuru wa kuamua bei, uhakika wa malipo yao pamoja na kuchochea ushindani kwa mazao ya wakulima nchini.  

Mabruki Said ambaye ni mmoja wa wakulima hao anasema kuwa msimu huu bei ni nzuri pia uuzaji ni wa uwazi na wenye kuleta maslahi mazuri kwa wakulima wa zao la korosho.

“Namshukuru Rais Samia na Waziri wa kilimo Mhe. Hussein Bashe kwa usimamizi mzuri wa uuzaji wa korosho kupitia mfumo wa TMX kwani tulivyokuwa tunauza awali na sasa, ni dhahiri kuwa mfumo huu unalenga kumnufaisha mkulima wa korosho” Mabruki Said.

Kwa upande wake Awadhi Niposa mmoja wa wakulima kutoka wilayani Newala anaahidi kuendelea kutoa ushirikiano juu ya ubora wa korosho kwa viongozi wake wa chama kikuu cha ushirika cha TANECU ili bei ziendelee kuwa juu kwani bei nzuri ya korosho huenda sambamba na ubora wake.

Wakulima hao wameyasema hayo wakati wa mnada wa tano wa chama kikuu cha Ushirika cha TANECU novemba 8, 2024 ambapo wameuza korosho zao kwa bei ya juu ya Tsh 3410 na ya chini ikiwa Tsh. 3210 kwa jumla ya tani 16,576 na kilo 765 kupitia mfumo wa TMX.

Related posts

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano wa kimataifa wa korosho uliofanyika Tanzania katika ukumbi wa Mikutano ya kimataifa wa Julius Nyerere

Peter Luambano

MATUMINZI YA SERIKALI MTANDAO KATIKA UTUNZAJI NYARAKA

Peter Luambano

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano wa kimataifa wa korosho uliofanyika Tanzania katika ukumbi wa Mikutano ya kimataifa wa Julius Nyerere

Peter Luambano