Uuzaji wa zao la korosho kupitia mfumo wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), mfumo ambao husimamia mnada kijiditali kwa lengo la kuwaongezea uhakika wa masoko, uhuru wa kuamua bei, uhakika wa malipo yao pamoja na kuchochea ushindani kwa mazao ya wakulima nchini wazidi kuleta matokeo chanya kwa wakulima wa Chama Kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao.
Katika mnada uliofanyika katika kijiji cha Ng’apa mkoani Lindi wakulima hao wameuza korosho zao kwa bei ya juu ya Tsh 3070/= na ya chini ikiwa Tsh 2830/=. Pia korosho za daraja la pili zimeuzwa kwa bei ya juu ya Tsh 2550/= na ya chini ikiwa Tsh 2510/= kwa jumla ya Tani 3,000 za korosho.
Kupitia TMX wakulima, wafanyabiashara, wauzaji bidhaa nje na watendaji wengine mbalimbali wanaweza kupata soko la ndani na la kimataifa na kupata bei nzuri katika kuuza au kununua bidhaa