Aprili 28, 2024 01:30
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

WADAU WAASWA KUZINGATIA UBORA KATIKA ZAO LA KOROSHO

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amewata wadau wote  wanaohusika kwenye mnyororo wa thamani wa zao la korosho nchini kussimamia ubora wa zao hilo kwenye uuzaji na usafirishaji ili kuliongezea thamani ndani na nje ya nchi.

Kanali Abbas amesema hayo Oktoba, 2023 kwenye kikao cha wadau wa masoko kilichofanyika katika jengo la ofisi za mkoa wa Mtwara, ambapo amewataka Bodi ya Korosho, vyama vikuu vya ushirika na warajisi kusimamia ubora wa zao la korosho kuanzia kwa mkulima mpaka kufika sokoni.


Aidha amewataka wasafirishaji na wanunuzi kutumia muda uliobaki kabla ya msimu kurekebisha mikataba ambayo kimsingi ndio inayokwenda kuhakikisha usalama na ubora wa bidhaa hiyo.

Akiongezea msisitizo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzana, Francis Alfred amewasihi wadau kuzingatia muongozo wa usimamizi wa udhibiti ubora wa korosho ghafi kwa msimu wa 2023/2024 ili kuendeleza thamani ya Korosho yetu katika soko la Dunia. Aidha Ndugu Francis ametoa onyo pia kwa wadau kuzingatia maagizo hayo yaliyopo kwenye muongozo na kuwasistiza waendesha maghala kuwa na wahihiki ubora waliopewa mafunzo na kupata leseni ya kazi hiyo na ikibainika mwendesha ghala kutumia mtu yeyote asiye na sifa atawajibika kulipa faini ya shilingi 500,000 kwa mhakiki ubora na huku mwendesha ghala kutozwa faini ya shilingi 1,500,000.

3 Oct.2023-Mtwara

Related posts

TAARIFA FUPI YA MINADA YA KOROSHO ILIYOFANYIKA TAREHE 21 OKTOBA, 2023 CHINI YA LINDI MWAMBAO KATIKA KITUMIKI AMCOS-LINDI MC.

Peter Luambano

KIKAO CHA SABA CHA BODI YA WAKURUGENZI ROBO YA TATU YA MWAKA

Peter Luambano

ZOEZI LA UHUISHAJI NA USAJILI WA KANZIDATA YA WAKULIMA LAZINDULIWA RASMI

Peter Luambano