Septemba 12, 2024 11:03
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

WAKULIMA WA KOROSHO KUENDELEA KUNEEMEKA NA PEMBEJEO ZA RUZUKU YA SERIKALI.

Wakulima wa Korosho nchini wataendelea kunufaika na pembejeo za ruzuku ya serikali kwaajili ya kuwakwamua na kuwaendeleza kiuchumi, hayo yamesemwa tarehe 18 Aprili 2024 katika uzinduzi wa upatikanaji na uzambazaji wa pembejeo kwa wakulima mwa msimu wa 2023/2024.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mhe. Mkuu wa wilaya ya Lindi SHAIBU NDEMANGA kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, ameishukuru Bodi ya Korosho Tanzania kwa uamuzi wa kuzindua usambazaji wa pembejeo kwenye Mkoa wake hususani kwa wakulima wa kata ya Kiwalala kwa niaba ya mikoa yote inayolima korosho nchini.

Pia Mhe. Ndemanga amei[ongeza Bodi kwa kazi kubwa inayoifanya na kutambua mchango mkubwa unaoletwa katika kuendeleza zao na kukuza kipato cha mkulima.

“Kabla ya pembejeo za ruzuku, wakulima walikuawakiuziwa pembejeo kwa bei kubwa na nyingi kati ya hizo zilikua pembejeo feki, Serikali kwa kuona umuhimu wa zao la Korosho iliamua kuingilia kati na kutoa pembejeo za ruzuku na kuhakikisha hakuna pembejeo feki nchini”Mhe.Ndemanga.

Hata hivyo tunaishukuru serikali ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo inafanya kwa wananchi wake kuendelea kutoa pembejeo za ruzuku kwa wakati na kupelekea kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho.

Aidha akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Mhe. Athuman Hongonyoko amewaasa wakulima kuacha kuendelea kuhudumia zao la Korosho kwa mazoea bali waangalie nyakati na mabadiliko ya hali ya hewa kwa sasa, “mvua zimekua nyingi tofauti na tulivyozoea, hivyo wakulima yatupasa kubadilika kutokana na hali ya hewa inavyobadilika” Mhe. Hongonyoko.

Akimkalibisha mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndugu Francis Alfred alisema kwa msimu wa 2023/2024, uzalishaji wa Korosho ulifikia tani laki tatu na tano (305,000).

Pia katika utekelezaji wa ahadi ya serikali ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kutoa pembejeo za ruzuku kwa wakulima wakorosho, mpaka sasa pembejeo zilizopo kwenye hifadhi za maghala ni tani 39,000 za dawa za unga na bado tani 30,000 zinaendelea kuletwa katika lengo lililowekwa kwa msimu wa 2023/2024.

Aidha aliwasihi wakulima kuwa wavumilivu wakati wa zoezi la usambazaji wa pembejeo hivyo maeneo yote yanayowahi katika uzalishaji tutaweka kipaumbele cha kwa kupeleka huko ili kunusuru na magonjwa.

Alimhakikishia Mgeni rasmi pembejeo zitapelekwa maeneo yote kwa wakati na kila mkulima aliyesajiliwa atapatiwa kile anacho stahili.

Kwa upande wa uboreshaji wa kanzidata ya wakulima, Francis alisema mpaka sasa wakulima 412,200 wamefikiwa ni sawa na aslimia 77 kati ya wakulima wote waliosajiliwa, uboreshaji wa taarifa unaendelea kwa kasi na Bodi itaendelea na zoezi hili kila muda pale uhitaji unapojitokeza.

Aliongeza kwa kuwasihi wakulima kuzingatia maelekezo yaliyotolewa wakati wa uhuishaji taarifa na kuhakikisha simu walizotumia kwenye taarifa zao zinatunzwa ili kufanikisha uchukuaji wa pemnbejeo wakati wa ugawaji.

Related posts

TAARIFA YA UTAFITI KUHUSU HALI YA UZALISHAJI WA KOROSHO NCHINI KWA MSIMU WA 2022/2023

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO YATOA JEZI ZA MICHEZO KWA JESHI LA ZIMAMOTO TANZANIA

Peter Luambano

KOROSHO QUEENS YAPATA UFADHILI WA VIFAA VYA MICHEZO

Peter Luambano