Mkurugenzi mkuu wa bodi ya korosho Tanzania ndg Fransis Alfred amesema kuwa bodi ya korosho kwa kushirikiana na vyama vya ushirika na wadau wengine katika kipindi hiki kuelekea minada mingine watazidi kusimamia ubora kuanzia vyama vya msingi hadi ghala kuu ili wakulima wengi wanufaike.
Ameyasema hayo wilayani newala mkoani mtwara wakati wa ufunguzi wa mnada wa kwanza wa mauzo ya korosho ambapo katika mnada huo bei ya juu iliyotangazwa ni tsh 4120 na bei ya chini ni tsh 4035 kwa kilo moja ya korosho ambapo jumla ya kilo 3857 zimeuzwa.
Ndg Francis amesema kuwa jumla ya makampuni45 yalikuwa tayari na leseni ambapo katika mnada huo jumla ya makampuni 37 yalishindana na korosho kununuliwa na makampuni10, huku 27 hayakupata.
Amefafanua kuwa kuwa hii ina maana kuwa uhitaji wa korosho ni mkubwa sana duniani na bei hizo ni kutokana na uhitaji wa korosho karanga katika soko la dunia kwani wanunuzi wengi katika msimu uliopita hawakuweza kununua korosho nyingi kutokana na kushuka kwa uzalishaji kwa hiyo Tanzania imekuwa na faida kubwa kuuza korosho huku kukiwa na uhitaji mkuwa duniani.
Pia katika mnada huo uliofunguliwa na mkuu wa mkoa wa mtwara kanali Patrick Sawala amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utoaji wa ruzuku za pembejeo buree kwa wakulima na huku akiwataka wakulima na wadau wengine wote waendelee kusimamia kwa ubora zao hilo.
Na kwa upande wao baadhi ya wakulima wameeleza kufurahishwa na bei hiyo ya korosho kwa msimu huu na kumshukuru Rais dkt. Samia suluhu Hassan kwa pembejeo walizozipata zilizowawezesha katika uzalishaji huo.