Septemba 12, 2024 10:36
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

TAARIFA YA UTAFITI KUHUSU HALI YA UZALISHAJI WA KOROSHO NCHINI KWA MSIMU WA 2022/2023

Kikao cha kujadili taarifa ya kitafiti ya kushuka kwa uzalishaji kilichojumuisha watafiti kutoka TARI Naliendele, Wataalamu wa kilimo CBT, wataalamu kutoka Mamlaka ya uthibiti wa afya ya mimea na viongozi wa vyama vikuu vya ushirika katika Ukumbi wa Mikutano wa Bodi ya Korosho Tanzania-Mtwara chini ya Mwenyekiti ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi Ndug.Hamidu Mponda leo tarehe 21 feb. 2023.

Katika tarifa hiyo ya matokeo ya kisayansi iliyofanywa na kituo cha utafiti wa mazao (TARI-Naliendele),moja ya sababu kubwa ikiwa ni hali ya hewa, lakini pia elimu ya matumizi ya Viuatilifu na mambo mengine kwa maeneo yote ya kitafiti ambayo imepelekea kuwa na uzalishaji duni wa korosho kwa msimu uliopita wa 2022/2023.

Katika tarifa hiyo,mambo machache kwa kifupi ni kama ifuatavyo:-

  1. Mabadiliko ya hali ya hewa;
  2. Kuwepo kwa masaa 16 ya kiwango cha chini cha muda wa kuwaka jua (sun shine hours) kwa kipindi cha mwezi wa nane na mwezi wa tisa. Hiki ni moja ya kigezo muhimu sana kinachopelekea mkorosho kutozalisha vizuri.
  3. Kuwepo kwa kipindi kirefu cha baridi hasa kwenye kipindi cha uzalishaji kilichopelekea baadhi ya mikorosho kutotoa maua kabisa na mingine yenye maua kukauka na kupukutika chini.
  4. Kuwepo kwa unyevu unyevu mwingi angani na mawingu mengi angani kumepelekea kuweka mazingira rafiki kwa mashambulizi ya magonjwa hasa kwa ugonjwa wa blaiti. Pia hali hiyo ilipelekea maua kutokufanya uchavushaji na hata kukauka na kudondoka.
  5. Matumizi ya viuatilifu yasiyotosheleza mahitaji halisi ya shamba, hii inatokana na wakulima wengi kukosa mitaji au kipato kwa ajili ya kuhudumia mashamba yao ikumbukwe kwamba baada ya msimu wa 2018/19 uzalishaji wa korosho ulishuka ikiwa ni sambamba na kuporomoka kwa bei ya korosho hadi kufikia wastani wa shilingi 2000 kwa kilo na baadhi ya wakulima wakiwa wamekopa fedha kutoka katika Taasisi mbalimbali za kifedha. Uwekezaji kwenye shamba la korosho hutegemea kwa kiasi kikubwa mapato ya msimu uliopita;
  6. Vilevile ucheleweshaji wa viuatilifu vilivyotolewa na serikali kwenye baadhi ya maeneo na kupelekea wakulima kutopuliza viuatilifu kwa wakati;
  7. Ukosefu wa mitaji kwa ajili ya kuhudumia mashamba ya korosho;
  8. Uchache wa mashine za kupulizia mikorosho na kupelekea uwepo wa foleni ya kupata huduma ya upuliziaji na hivyo kusababisha kutokupulizia viuatilifu kwa wakati;
  9.  Matumizi ya mashine za upuliziaji zenye uwezo mdogo (chini ya nguvu farasi 5 (HP) ambazo zinashindwa kupeleka viuatilifu katika maeneo ya juu ya mkorosho.

Aidha wataalamu wote kwa pamoja wameishauri serikali kushughulikia mapungufu yaliyojitokeza ambayo yapo chini ya Mamlaka yake ili kuondoa sintofahamu kwa misimu ijayo.

Related posts

RATIBA YA MINADA KWA MSIMU WA 2023/2024

Peter Luambano

TAARIFA FUPI YA MINADA YA KOROSHO ILIYOFANYIKA TAREHE 20 OKTOBA. 2023 A.TANECU LTD KATIKA UKUMBI WA TANDAHIMBA DC

Peter Luambano

TAARIFA KWA WADAU WOTE WA TASNIA YA KOROSHO NCHINI/ NOTICE TO ALL STAKEHOLDERS IN THE CASHEWNUT INDUSTRY

Peter Luambano