Aprili 23, 2024 03:05
Bodi ya Korosho Tanzania
Matukio

PEMBEJEO BILA MALIPO KWA WAKULIMA

Bodi ya korosho Tanzania imezindua zoezi la usambazaji wa pembejeo na Mabomba bila malipo zilizotolewa na Serikali Chini ya Uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluuhu Hassan kwa wakulima wakorosho Kwa maeneo yote ya uzalishaji Nchini.

Akiongoza Zoezi hilo la Kitaifa,Mgeni rasmi ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti,amewahakikishia wakulima na wadau wote wa korosho Nchini kwamba,hakuna chupa au tone hata moja litakalo potea bila kumfikia mkulima,akisisitiza kauli hiyo,Brig.Jen. Gaguti amesema” sitarajii kuona mtu au kikundi chochote kikijaribu kukwamisha zoezi hili kwa namna yeyote ile, na kwa yeyote atakae jaribu kuthubutu,hatua kali zitachukulia na nitashughulika nao mwenyewe watu au mtu yeyote bila huruma”.

Akiongezea msisitizo wa kauli ya mgeni rasmi,Mwenyekiti wa Bodi Ya korosho Tanzania Brigedia Jenerali Mstaafu,Aloyce Mwanjile, amesema “kumekuwepo na tabia ya watu kufanya vitu kwa mazoea,kwasasa hatutaacha kuchukua hatua thabiti kwa watu wote watakaolenga kukwamisha kufikisha lengo la uzalishaji,mimi ni Mstaafu,lakini bado sijatupa Unifomu zangu,na ikibidi nitazivaaa ili kuhakikisha napambana na mtu au kikundi cha watau wenye nia ovu”.

Akitoa shukrani kwa Mgeni rasmi,mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara,ameapa kutoa ushirikiano mpaka mwisho wa zoezi hili na kuhakikisha atashiriki kusimamia zoezi hili kwa kushirikiana na Kamati ya ugawaji wa Pembejeo mpaka tone la mwisho na kuhakikisha kila pembejeo inamfikia mkulima pale alipo bila kupotea.

Hafla hii ya uzinduzi imefanyika mapema tarehe 17 Mei 2022 mjini Mtwara eneo la Ghala la kuhifadhia Pembejeo zilizohifadhiwa katika Bandari ya Mtwara.

Related posts

BODI YA KOROSHO YAZINDUA RASMI MKUTANO WA KIMATAIFA WA KOROSHO 11-13 OCTOBA 2023 JNICC-DAR ES SALAAM

Peter Luambano

ELIMU YA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA UKIMWI KWA WAFANYAKZI WA BODI YA KOROSHO

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO NA MWENDELEZO WA UBORESHAJI WA KANZI DATA YA WAKULIMA WA KOROSHO NCHINI

Peter Luambano