Julai 20, 2024 08:01
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BODI YA KOROSHO NA MWENDELEZO WA UBORESHAJI WA KANZI DATA YA WAKULIMA WA KOROSHO NCHINI

Maafisa wa Bodi ya korosho Tanzania wakiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mbele ya Katibu Tawala wa wilaya Ndug. Milongo Sanga kwa utambulisho rasmi wa kazi ambayo ni mwendelezo wa uboreshaji wa taarifa za Wakulima wa Korosho kwenye kanzi data kwa Wilaya ya Tunduru.

Aidha zoezi hili linaendelea Nchi nzima kwa Mikoa yote inayolima korosho na kwa sasa limeanzia Mkoa wa Lindi, Ruvuma na Mtwara kwa Wilaya za Tunduru, Ruangwa, Masasi na Lindi

Akiongea katika utambulisho wa maafisa hao, Katibu Tawala amepongeza hatua ambazo Bodi ya korosho imechukua na kuongeza kwamba zoezi hili litaenda kupunguza baadhi ya changamoto zilizojitokeza msimu uliopita hasa katika ugawaji wa Pembejeo kupitia taarifa za usajili wa mkulima.

Akitoa neno la shukrani kwa Katibu Tawala huyo,Mejena wa Bodi ya Korosho Tawi la Tunduru, Bi. Shauri Mokiwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho, ameiomba Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Tunduru kuhamasisha Wakulima wote wa Korosho kujitokeza kwa wakati na kuhuisha taarifa zao ili ziweze kutumika katika mipango endelevu ya zao la Korosho hususani katika zoezi la ugawaji wa viuatilifu vya ruzuku.

Related posts

ZOEZI LA UHUISHAJI NA USAJILI WA KANZIDATA YA WAKULIMA LAZINDULIWA RASMI

Peter Luambano

ELIMU YA MAZINGIRA NA HEWA YA UKAA KWA BODI YA WAKURUGENZI

Peter Luambano

CATALOGUE 2 CORECU

Peter Luambano