Septemba 12, 2024 10:50
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

MKUTANO MKUU WA WADAU WA TASNIA YA KOROSHO 2024

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amefungua Mkutano Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Korosho 2024 leo tarehe 22 Agosti 2024 na kuwatia moyo wadau wa tasnia hiyo kuwa Serikali itaendelea na mikakati yake ya kuweka utaratibu wa kusimamia ubanguaji nchini. Ameongeza kuwa mauzo ya korosho zilizobanguliwa kwenda nje ya nchi yameshaanza kwa mara ya kwanza hususan katika nchi za Ulaya.

Waziri Bashe amewashukuru Viongozi wa wa Mikoa na Wilaya zinazolima korosho ikiwemo Mtwara, Lindi, Tanga, Pwani, Dodoma na Singida, wakulima, wafanyabiashara na wadau katika mnyororo wa thalami wa tasnia ya korosho kwa kushiriki Mkutano huo muhimu unaofanyika katika Jengo la PSSSF, mkoani Dodoma.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho, Bw. Francis Alfred ameeleza kuwa malengo ya tasnia hiyo ni kuongeza uzalishaji wa korosho kutoka tani 310,000 kwa mwaka 2023/2024 hadi kufikia tani 1,000,000 mwaka 2030 ili kuongeza thamani ya zao, kupanua wigo wa masoko katika soko la ndani ya nchi, Asia, Mashariki ya Kati na Marekani.

Aidha, imeelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Thomas Bwana kuwa tafiti mbalimbali za kuboresha zao la korosho, mbegu, viuatilifu zinaendelea ili kuongeza ubora wa Korosho kwa kulingana na uhitaji wa masoko lengwa.

Related posts

TANECU WAUZA KOROSHO ZOTE KILO 3,666,570 DESEMBA 2,2022

Peter Luambano

FURSA ZA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA

Peter Luambano

KIKAO CHA TATHMINI YA UZALISHAJI, MASOKO NA UBANGUAJI WA KOROSHO MSIMU WA 2023/2024

Peter Luambano