Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndg. Francis Alfred ametoa ufafanuzi juu ya malipo ya wakulima wa Korosho nchini katika kuelekea msimu huu wa mwaka 2024/2025.
Ndg. Alfred amesema Wanunuzi wa Korosho watalipa fedha kwa vyama vikuu vya ushirika ndani ya siku 5 baada ya mnada kufanyika na Vyama vikuu vinatakiwa kukamilisha malipo hayo kwa wakulima ndani ya saa 48 ambayo ni sawa na siku 2 ili wakulima wapate fedha zao za mauzo, hivyo mkulima atapata malipo yake siku 7 baada ya mnada kufanyika.
Mnada wa kwanza wa Korosho nchini kwa msimu wa mwaka 2024-2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 11,2024 kwa kuanzia na chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU.