Januari 14, 2025 12:25
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

SERIKALI KUENDELEA KUTOA RUZUKU ZA PEMBEJEO BUREE KWA WAKULIMA WA KOROSHO

Waziri wa kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema kuwa serikali itaendelea kutoa ruzuku za pembejeo kwa wakulima wa korosho nchini buree.

Bashe ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Maranje mkoani Mtwara octoba 1,2024 na kuwa mpango wa serikali ni kuuza korosho ya ndani ya nchi baada ya kubanguliwa ifikapo 2026/2027.

Vilevile ameitaka bodi ya korosho kupitia Mkurugenzi wake mkuu ndg. Francis Alfred kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati stahiki na kuwa katika msimu ujao wa korosho tani elfu tatu za korosho zibanguliwe kwenye kiwanda cha Maranje.

Naye Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya korosho Tanzania ndg. Fransis Alfred amesema kuwa mradi huo utazalisha ajira takribani elfu thelathini ifikapo 2027 mara baada ya mradi huo kukamilika na kuongeza kuwa utawanufaisha wananchi wa Maranje na Watanzania kwa ujumla.

Related posts

SERIKALI YAJIPANGA KUMUINUA KIUCHUMI MKULIMA WA KOROSHO

Amani Ngoleligwe

KOROSHO MARATHON YAFIKA KILELENI KWA SHANGWE

Amani Ngoleligwe

Kikao cha ufunguzi wa zoezi la ukaguzi wa hesabu za taasisi Kwa mwaka 2021/2022

Peter Luambano