Febuari 13, 2025 09:16
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari Zinazojiri

MAPOKEZI YA VIWATILIFU MKOANI MTWARA

Viuatilifu vya zao la Korosho vimeanza kupokelewa mkoani Mtwara, ambapo kampuni ya Bens agro star imeleta lita 100,000 na Suba agro lita 187,000 kwa ajili ya kutibu ubwiri unga na bright na lita 20,000 kwa ajili ya kuua wadudu.

 Kwa upande wa sulphur ya unga tayari tan 1,750 imepokelewa mkoani humo.

Kulingana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred anasema hatua hiyo itapelekea kuanza ugawaji wa viwatilifu vya korosho katikati ya mwezi Aprili,2022.

Hata hivyo mahitaji kwa mwaka huu yameongezeka kwa asilimia 60 ambapo Viuatilifu vya maji ni Lita milion1.5 sulphur ya unga tani 25,000 na mabomba ya kupulizia 35,000.

Mwaka jana mahitaji yalikuwa sulphur ya unga ilikuwa tani 15,000 na viuatilifu vya maji lita elfu 9,000.

Related posts

NAIBU WAZIRI SILINDE AZINDUA MIRADI KATIKA SEKTA YA KILIMO

Amani Ngoleligwe

SHILINGI BILIONI 743.57 /= ZAPATIKANA MAUZO YA KOROSHO MSIMU WA 2024/2025

Amani Ngoleligwe

TANI 180,342 ZA KOROSHO ZAUZWA NDANI YA WIKI TATU MSIMU WA 2024/2025.

Amani Ngoleligwe