
Katika maonyesho hayo washiriki 520 walikadiriwa kushiriki moja kwa moja na watu takribani 15,000 kujionea bidhaa zinazozalishwa kupitia viwanda na fursa zinazopatikana Mkoani humo.
“Maonyesha haya yameratibiwa na TANTRADE kwa kushirikiana na Shirika linalohudumia viwanda vidogo vidogo( SIDO )Kanda ya Mashariki”,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Abubakari Kunenge akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki kufanikisha maonyesho hayo.