Oktoba 17, 2025 10:24
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BODI YA KOROSHO TANZANIA (CBT) YAWATAKA WAKULIMA KUENDELEA KUDUMISHA UBORA WA KOROSHO.

Wakati minada ya korosho ikiwa inaendelea mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania ndg Francis Alfred Alfred amewataka wakulima wa korosho nchini kuendelea kudumisha ubora wa korosho ili kuhakikisha kuwa bei ya korosho ghafi inaendelea kuwa nzuri.

Ndg. Alfred ameyasema hayo wakati wa mnada wa kwanza wachama kikuu cha ushirika cha Mtwara, Masasi na Nanyumbu (MAMCU) uliofanyika katika Kijiji cha Nakachindu wilayani Masasi mkoani Mtwara ocktoba 14-2024.

Katika mnada huo wakulima waliuza korosho zao kwa bei ya juu ya Tsh 4195 na bei ya chini ikiwa Tsh 3440, jumla ya tani 18,000 ziliuzwa kupitia mfumo wa soko la bidhaa Tanzania (TMX)

Wakieleza furaha yao ya kuuza korosho zao kwa bei ya juu baada ya miaka kadhaa, wamemshukuru Rasi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa utoaji wa pembejeo buree, ambao umewawezesha kupata uzalishaji mzuri wa korosho katika msimu huu wa 2024/2025.

Pia wamemshukuru waziri wa kilimo Hussein Bashe kwa kusimamia na kuhakikisha maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwainua wakulima wa korosho yanatekelezwa ipasavyo.

Related posts

TANGAZO LA MAFUNZO YA UDHIBITI UBORA WA KOROSHO GHAFI MSIMU 2025/2026 KWA WADAU WA TASNIA YA KOROSHO NCHINI.

Amani Ngoleligwe

RATIBA YA MINADA KWA MSIMU WA 2024/2025

Amani Ngoleligwe

JARIDA LA KOROSHO MWEZI AGOSTI 2023

Peter Luambano