Julai 19, 2025 02:51
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

TANECU WAUZA KOROSHO KWA BEI YA JUU TSH. 3760/= NA BEI YA CHINI TSH.3540/=, UBORA WASISITIZWA.

Katika kuhakikisha wakulima wa zao la korosho wanazidi kunufaika na kilimo chao kupitia minada inayoendelea, bodi ya korosho Tanzania imewataka wakulima hao kusimamia ubora wa korosho zao.

Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania ndg. Francis Alfred oktoba 18, 2024 wakati wa mnada wa pili wa chama kikuu Cha ushirika TANECU wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.

Ndg. Alfred amesema kuwa ili kuhakikisha kila mkulima ananufaika na bei nzuri ya msimu huu anatakiwa kupeleka ghalani korosho iliyokauka vizuri kwani mnunuzi hutoa bei kulingana na ubora wa korosho.

Katika mnada huo wakulima wameuza korosho zao kwa bei ya juu ya Tsh 3760/= na bei ya chini ikiwa Tsh 3540/= kwa jumla ya tani 20335 na kilo 417 ambazo zimeuzwa kupitia mfumo wa soko la bidhaa Tanzania (TMX).

Related posts

JARIDA LA KOROSHO MWEZI AGOSTI 2023

Peter Luambano

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KWA WAKULIMA WA KOROSHO

Peter Luambano

MKUU WA MKOA WA MTWARA AZINDUA MINADA YA KOROSHO KWA MSIMU WA 2022/2023 LEO TAREHE 21 OKTOBA KWA VYAMA VIKUU VIWILI TANECU NA MAMCU MKOANI MTWARA.

Peter Luambano