Febuari 16, 2026 02:52
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BODI YA KOROSHO YATOA MASHINE ZA UBANGUAJI KOROSHO

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania ndg. Francis Alfred amekabidhi mashine nne za kubangulia korosho kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mhe. Shadida Ndile na diwani wa viti maalum Mhe. Zuhura Mikidadi ikiwa ni sehemu ya kuongeza jitihada za kukuza ubanguaji wa korosho nchini kwa wajasiriamali.

Ndg. Alfred amesema kuwa moja ya jukumu la bodi ya korosho ni kuisaidia jamii katika kuipatia vitendea kazi, pia amemtaka mstahiki meya kuijulisha bodi ya korosho endapo kutakuwa na uhitaji zaidi ambapo utaandaliwa utaratibu maalum wa kupatiwa mashine hizo kwani pia Bodi ya Korosho inatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ubanguaji wa korosho nchini Tanzania ni sehemu muhimu katika sekta ya kilimo inayochangia kuongeza thamani ya zao la korosho, na kutokana na uhalisia kuwa Tanzania huzalisha korosho zenye ubora wa hali ya juu, serikali imewekeza katika ujenzi wa viwanda vya ubanguaji, lengo likiwa ni kuongeza thamani ndani ya nchi na kupanua ajira, hasa kwa vijana na wanawake.

Kwa miaka ya hivi karibuni, juhudi zimeongezeka kupitia ushirikiano wa Serikali pia Bodi ya Korosho Tanzania na Kwa kuongeza uzalishaji wa korosho zilizobanguliwa, Tanzania inalenga kuongeza mapato ya wakulima, kupanua masoko ya nje, na kushindana katika soko la kimataifa la bidhaa zilizoongezwa thamani.

Related posts

KATIBU MKUU MWELI AKUTANA NA BALOZI WA ITALIA

Amani Ngoleligwe

UHUISHAJI TAARIFA ZA WAKULIMA WA KOROSHO WAENDELEA KWA MAFANIKIO KATIKA KATA YA NYANGAO MKOANI LINDI

Amani Ngoleligwe

ELIMU YA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA UKIMWI KWA WAFANYAKZI WA BODI YA KOROSHO

Peter Luambano