Julai 11, 2025 03:17
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

VIONGOZI CBT WAKUTANA NA WAGENI KUTOKA UHOLANZI KUJADILI UONGEZAJI THAMANI ZAO LA KOROSHO

VIONGOZI CBT WAKUTANA NA WAGENI KUTOKA UHOLANZI KUJADILI UONGEZAJI THAMANI ZAO LA KOROSHO

Kikao muhimu kimefanyika kati ya viongozi wa Bodi ya Korosho Tanzania, wageni mashuhuri kutoka Uholanzi pia wabanguaji wa korosho wanaouza korosho zilizoongezwa thamani katika soko la Uholanzi ambapo mazungumzo yalijikita katika uongezaji thamani wa zao la korosho kwa ajili ya soko la Uholanzi, linaloendelea kuwa na mahitaji makubwa ya bidhaa hizi zenye ubora wa hali ya juu.

Katika kikao hicho, wajumbe wamejadili fursa za kuongeza thamani katika mnyororo wa uzalishaji wa korosho huku wageni kutoka Uholanzi wakionyesha kuridhishwa na jitihada za Tanzania katika ubanguaji wa korosho pamoja na ubora wa zao hilo linazozalishwa nchini.

Ni dhahiri kuwa Ushirikiano huu wa kibiashara kati ya Tanzania na Uholanzi kwa kupitia mikakati madhubuti ya kuongeza thamani, unaongeza mwanga katika tasnia ya Korosho nchini, na hii itakuwa na manufaa zaidi kwa taifa kupitia mapato ya mauzo ya nje na nafasi za ajira zitakazotokana na viwanda vya ndani.

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Bodi ya Korosho Tanzania novemba 22-2024, hivyo uzalishaji na usafirishaji wa korosho zilizoongezwa thamani utazidi kuimarishwa huku pia wakulima wa korosho wakizidi kunufaika kupitia kilimo chao.

Related posts

MATUMINZI YA SERIKALI MTANDAO KATIKA UTUNZAJI NYARAKA

Peter Luambano

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA RUFIJI LATEMBELEA BODI YA KOROSHO MTWARA.

Peter Luambano

VITUO VYA KAZI VYA MAAFISA UGANI KILIMO 500

Amani Ngoleligwe