Disemba 11, 2024 10:12
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BODI YA KOROSHO YATOA JEZI ZA MICHEZO KWA JESHI LA ZIMAMOTO TANZANIA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndg.Reuben Putaputa amekabidhi Jezi za Mpira wa Miguu pamoja na Mipira kwa Jeshi la Zimamoto Tanzania Mkoani Mtwara.

Makabidhiano haya yamefanyika katika Ofisi za Bodi ya Korosho Makao Makuu Mtwara tarehe 27 Machi 2023, aidha kwa kutambua mchango wa jeshi hili katika kulinda usalama na majanga eneo la kazi,Bodi ya Korosho imeona ni vyema kutekeleza zoezi hili ili kuwajengea Afya itokanayo na Michezo lakini pia kuboresha mahusiano na mshikamano katika kujenga Taifa letu.

Akipokea jezi hizo kwa niaba ya Jeshi la Zimamoto Tanzania, Inspekta Elizabeth Mpondela ameishukuru Bodi na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika kila jambo ili kuhakisha usalama sehemu za kazi inakua ni kipaumbele.

Related posts

SERIKALI YAJIPANGA KUMUINUA KIUCHUMI MKULIMA WA KOROSHO

Amani Ngoleligwe

TAARIFA FUPI YA MINADA YA KOROSHO ILIYOFANYIKA TAREHE 20 OKTOBA. 2023 A.TANECU LTD KATIKA UKUMBI WA TANDAHIMBA DC

Peter Luambano

RAIS DKT SAMIA ASHIRIKI MIKUTANO MUHIMU KUHUSU KILIMO-MAREKANI

Amani Ngoleligwe