Aprili 19, 2024 04:08
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

ZOEZI LA UHUISHAJI NA USAJILI WA KANZIDATA YA WAKULIMA LAZINDULIWA RASMI

Katika kuhakikisha Serikali inafikia lengo la kuongeza uzalishaji wa korosho ghafi nchini kufikia tani 700,000 ifikapo mwaka 2025/2026. Ili kufikia lengo hilo Serikali haina budi kuboresha kanzidata ya wakulima itakayosaidia kupanga mipango mbalimbali ya uendelezaji zao ikiwa ni pamoja na ununuzi na usambazaji wa pembejeo, ugawaji wa mbegu na miche bora ya korosho, vifungashio (magunia), huduma za ugani, ubanguaji, utafiti na masoko. Aidha, itakumbukwa kwamba Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe alipokuwa akihitimisha hotuba yake ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 alisisitiza umuhimu wa Bodi ya korosho kuhuisha kanzidata ya wakulima.

Kwa muktadha huo, Bodi ya Korosho kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali ngazi ya Mikoa na Wilaya itatumia Mfumo wa Kielektroniki wa Usajili wa Wakulima ulioandaliwa na Wizara ya Kilimo katika uhuishaji wa kanzidata ya wakulima wa korosho nchini. Zoezi hilo litafanyika katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itahusisha Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga; na awamu ya pili itafanyika katika Mikoa mipya.

Uhuishaji wa kanzidata utatumia vitabu pamoja na simu janja ambazo zimeunganishwa na Mfumo maalum wa usajili wenye uwezo wa kuchukua alama za vidole, kupima ukubwa wa mashamba pamoja na idadi ya mikorosho.

Zoezi hili litafanyika ngazi ya Kijiji na kusimamiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo kila mkulima atahitajika kuhuishwa taarifa zake akiwa shambani.

Akiongea katika uzinduzi huo uliofanyika tarehe 04 Januari, 2023 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara, Kata ya Naliendele, Mtaa wa Sogea,Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed mbele ya wageni waalikwa,waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Mtwara, Waheshimiwa wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Wilaya  za Mkoa wa Mtwara, Wenyeviti na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Mtwara, Maafisa Kilimo wa Halmasahuri za Mkoa wa Mtwara na Viongozi wa chama,amesisitiza kuwepo kwa mwendelezo wa zoezi hili la usajili na kuleta matoke chanya kama ilivyokusidiwa.

Aidha,Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Brig.General Mstaafu Aloyce Mwanjile,amewaomba na kuwasisitiza wakulima Nchi nzima kwa Mikoa inayozalisha korosho kujitokeza na kutoa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hili na kurahisha upatikanaji wa takwimu sahihi ya makadirio ya utoaji huduma za ugani na pembejeo kwa urahisi kwa wakulima waliosajiliwa na kutambuliwa kwenye kanzi Data. Akisisitiza kauli ya mwenyekiti wa Bodi,Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korsoho Tanzania Ndugu Francis Alfred alisema,hakuna Mkulima wa korosho atakaepata pembejeo za ruzuku iwapo hajatambuliwa kwenye kanzi data ya wakulima kutokana na kutowekuwepo kwa taarifa zake na hivyo kutopangwa kwenye bajeti, “bajeti hupangwa kadili ya idadi ya wakulima na taarifa zao sahihii zitokanazo na kanzi data hii”.

Related posts

KIKAO CHA SITA CHA BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA KOROSHO TANZANIA

Peter Luambano

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano wa kimataifa wa korosho uliofanyika Tanzania katika ukumbi wa Mikutano ya kimataifa wa Julius Nyerere

Peter Luambano

JARIDA LA KOROSHO MWEZI AGOSTI 2023

Peter Luambano