Oktoba 11, 2024 05:57
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

KIKAO CHA SABA CHA BODI YA WAKURUGENZI ROBO YA TATU YA MWAKA

Bodi ya Korosho Tanzania imeendelea na vikao vyake vya kisheria vya Bodi ya Wakurugenzi kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa serikali, kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Brig.Gen. Mstaafu Aloyce Damian Mwanjile tarehe 5 Januari 2023 Mjini Mtwara kikiwa na ajenda mbalimbali.

Kati ya ajenda zilizojadiliwa ni pamoja na kupitisha na kuidhinisha taarifa ya Bodi kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka, kujadili changamoto zilizojitokeza na zinazoendelea kujitokeza sambamba na kupitisha maombi kwa ajili ya utekelezaji wa mpango kazi wa Bodi kwa robo ya tatu ya mwaka.

Aidha kikao kimepitia na kujadili kwa kina taarifa za kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya kuendeleza zao, kamati ya ukaguzi pamoja na kamati tendaji, mwenyekiti amezipongeza kamati zote kwa taarifa zao na pia kusisitiza kuwepo na mipango maalum kwa Bodi kufanya kazi yake kwa bidii na maarifa lakini pia kwa uwazi ili jamii iwe na uelewa na utendaji kazi wa Bodi ya Korosho Tanzania.

Aidha Mwenyekiti ametumia kikao hiki kutoa taarifa  ya uteuzi rasmi wa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Ndug. Francis Alfred ambae kwa sasa amethibitishwa na kuwa Mkurugenzi Mkuu kwa kipindi cha Miaka mitano.

Pia amesisitiza Bodi iendelee kutafuta soko la Korosho hususani kwa Korosho zilizobanguliwa ili wakulima wanufaike na Kilimo cha Korosho.

Related posts

HALI YA SOKO LA KOROSHO GHAFI KWA MWAKA 2022/2023

Peter Luambano

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano wa kimataifa wa korosho uliofanyika Tanzania katika ukumbi wa Mikutano ya kimataifa wa Julius Nyerere

Peter Luambano

FURSA ZA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA

Peter Luambano