April 1, 2023 01:59
Bodi Ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriMatukioSlider

KIKAO CHA SITA CHA BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA KOROSHO TANZANIA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Brig. Gen. (Mstaafu) Aloyce Damian Mwanjile ndc ameongoza kikao cha Bodi ya Wakurugenzi tarehe 19 Oktoba 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Korosho Tanzania kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu Mtwara
Menejimenti imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazigo ya kikao kilichopita, taarifa ya utekelezaji wa robo ya kwanza, mipango ya utekelezaji kwa robo ya pili ya mwaka 2022/2023. Pia Bodi imepitia utekelezaji wa maagizo ya viongozi yaliyotolewa huko nyuma ikiwa ni pamoja na maandalizi ya msimu wa mauzo ya korosho ya mwaka 2022/2023.
Akiongea katika kikao hicho, Mwenyekiti amesisitiza kuongeza ufanisi katika kutekeleza shughuli zilizopangwa na kupitishwa ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa.
Sambamba na hayo, Mwenyekiti ameipongeza Menejimenti kwa uwajibikaji mzuri katika kutimiza majukumu yao ya kazi.

Related posts

TANZANIA YAPATA SOKO JIPYA LA KOROSHO BARANI ULAYA

Peter Luambano

TANGAZO LA RATIBA YA KUANZA KWA MINADA YA KOROSHO GHAFI KUPITIA VYAMA VYA USHIRIKA KATI YA TAREHE 21-23 OCTOBA 2022

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO TANZANIA YASHIRIKI WIKI YA UWEKEZAJI NA BIASHARA MKOANI PWANI

Peter Luambano