Septemba 12, 2024 10:44
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

TANZANIA YAPATA SOKO JIPYA LA KOROSHO BARANI ULAYA

Bodi ya korosho Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeendelea na juhudi za kuhakikisha wakulima wanafaidika na za zao hili katika maeneo yao hususani kwa kuongeza ajira na kipato kwa kila mkulima wa korosho  Nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo,Kaimu Mkurugenzi Mkuu Ndg.Francis Alfred amesema, juhudi hizi zinatokana na mpango thabiti wa kuongeza kiwango cha korosho inayobanguliwa hapa Nchini hivyo kupelekea ongezeko la thamani ya korosho tofauti na usafirishaji wa korosho ghafi,matokea ya mpango huu ni pamoja na uzinduzi wa usafirishaji wa Korosho zilizobanguliwa kupitia Viwanda vidogovidogo na Vikundi vya wajasiliamali wilayani Tandahimba waastani wa Tani 26 za korosho na Tani Moja ya Nyama ya korosho ambazo zimetafutiwa soko jipya barani Ulaya katika Nchi za Uholanzi na Ujerumani.

Kati ya Tani 26 za korosho hizi,tani 12 na tani moja ya nyama ya mabibo zinasafirishwa kwenda Ujerumani kutoka kikundi cha kina Mama cha TANZANIA DELICIOUS CASHEWS LTD na Tani 14 zinasafirishwa kwenda Nchini Uholanzi kutoka kiwanda cha AMAMA FARMS COMPANY LIMITED,vyote hivi viko wilaya ya Tandahimba-Mtwara.

Akizindua usafirishaji huo,Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba  Mheshimiwa Kanali Patric Swala amesema, nifaraja kubwa kuona mambo kama haya yameanza kujitokeza kwa Nchi yetu na yote hii inatokana na juhudi za serikali yetu pendwa chini ya Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassani,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Related posts

KUTOKA URAMBO-TABORA:Mzee Ibrahim Kadete kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mkoa wa Tabora mkulima wa korosho tangu mwaka 2017 akiwa katika shamba lake.

Peter Luambano

Mh DUNSTAN KYOBA AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA BODI YA KOROSHO.

Peter Luambano

TICC-WAJUMBE WAKIWA KWENYE MKUTANO JNICC DAR ES SALAAM

Peter Luambano