Chama kikuu cha ushirika wilaya Tandahimba na Newala (TANECU) tarehe 2 Desemba 2022, kimeuza korosho zote zilizopelekwa mnadani kwa bei ya chini ya Shilingi 1930 na Bei ya juu ya Shilingi 1990.
Korosho zilipelekwa mnadani zilikua kilo 3,666,570 zote zikiwa na ubora wa daraja la kwanza (SOT 51-52),uhitaji wa soko kwa wanunuzi ulikua kilo 7,305,000 kati ya wanunuzi 19 waliohudhuria mnada huo na kufanya korosho zote zilizoletwa sokoni kununuliwa kwa bei kati ya Shilingi 1930 mpaka Shilingi 1990