Febuari 22, 2024 11:06
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

BODI YA KOROSHO NA TARI WAFANYA KIKAO CHA PAMOJA

Bodi ya Korosho (CBT) na kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania-Naliendele (TARI) wamekutana na kufanya kikao cha pamoja katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara tarehe 20 Machi, 2023.

Lengo kuu la kikao hicho ni kuimarisha mahusiano zaidi ya kiutendaji katika uendelezaji wa tasnia ya Korosho Tanzania,ikumbukwe kuwa taasisi hizi zote zipo chini ya wizara ya Kilimo na zinamajukumu tofauti ikiwa ni kusimamia,kuendeleza na kukuza tasnia ya Korosho.

Kupitia kikao hiki, mwenyekiti wa kikao ambae pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI-Nalendele Dkt. Fortunus A.Kapinga; ameelezea namna TARI inavyofanya kazi lakini pia mchango wa TARI katika uendelezaji wa zao la Korosho Tanzania.

Dkt.Kapinga amesisitiza zaidi ushirikiano baina ya watumishi wa TARI na Bodi ya Korosho katika utendaji kazi ukizingatia taasisi zote mbili zinamalengo sawa kwenye kuendeleza,kusimamia na kukuza zao la Korosho.

Kupitia kikao hicho,Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti mwenza wa kikao Ndg. Francis Alfred,ameiomba TARI kusaidia tasnia ya Korosho hasa katika kufanya tafiti nyingi ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili zao la Korosho.

Related posts

KUTOKA URAMBO-TABORA:Mzee Ibrahim Kadete kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mkoa wa Tabora mkulima wa korosho tangu mwaka 2017 akiwa katika shamba lake.

Peter Luambano

SALES CATALOGUE – AGROFOCUS NEWALA

Peter Luambano

BODI YA KOROSHO YAPEWA ELIMU YA RUSHWA

Peter Luambano