Januari 13, 2025 11:00
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

TASNIA YA KOROSHO YAZIDI KUCHANGIA UCHUMI NCHINI

Tasnia ya korosho nchini Tanzania imeendelea kuwa moja ya tasnia muhimu inayochangia katika uchumi wa nchi. Serikali imewekeza katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji Pamoja na utoaji wa pembejeo buree kwa wakulima. Hii imesaidia kuongeza uzalishaji na ubora wa korosho, na hivyo kuongeza mapato kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani.

Ongezeko la bei ya korosho katika msimu huu wa 2024/2025 limeleta manufaa kwa Tanzania, kwani nchi inazalisha na kuuza korosho kwa wingi, hasa katika masoko ya kimataifa. Hali hii imeongeza ajira na kuboresha maisha ya wakulima wa korosho, hasa katika mikoa ya Lindi, Mtwara, na Ruvuma.

Hata hivyo, serikali imetangaza mikakati ya kuboresha usimamizi wa soko la korosho, ili kuepuka changamoto za kuuza korosho kwa bei ya chini, na hivyo kuiwezesha tasnia hii kuendelea kuwa na mafanikio makubwa.

Tarehe 4 disemba 2024, kimefanyika kikao kati ya wafanyabiashara wanaouza korosho nje ya nchi na uongozi wa Bodi ya korosho Tanzania wakijadili namna ya kuwalinda wafanyabiashara wa ndani katika soko la dunia na mengine mengi yahusuyo tasnia ya korosho kwa msimu huu wa 2024/2025.

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Bodi ya korosho Tanzania kikiongozwa na Mkurugenzi wa Masoko na Udhibiti Ubora ndg. Revelian S. Ngaiza.

Related posts

TANGAZO LA KAZI

Peter Luambano

BEI YA JUU YA KOROSHO YALETA SHANGWE KWA WAKULIMA KATIKA MNADA WA KWANZA MKOANI MTWARA

Amani Ngoleligwe

JARIDA LA KOROSHO MWEZI AGOSTI 2023

Peter Luambano