Agosti 28, 2025 08:02
Bodi ya Korosho Tanzania
Habari ZinazojiriKiteleziMatukio

KATIBU MKUU MWELI AKUTANA NA IFAD, AFDP

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na wataalamu kutoka Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) wakiongozwa Mkurugenzi Mkazi, Bw. Mohammed Al-Ghazaly pamoja na Mratibu wa Programu hiyo Bw. Stephano D. Mgani.

Mazungumzo hayo yamefanyika tarehe 06 Novemba, 2024, na kulenga ufuatiliaji wa utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), ambayo pia ni Programu inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu.

Aidha, Wataalamu hao wameeleza kufurahishwa na utekelezaji wa programu tangu kuanzishwa kwake mwaka 2022 anbapo umechangia ongezeko la uzalishaji wa mbegu na uwekaji wa miundombinu katika mashamba ya mbegu ili kuwa na kilimo chenye tija kwa wakulima.

CHANZO: Wizara ya Kilimo

Related posts

BODI YA KOROSHO YAPEWA ELIMU YA RUSHWA

Peter Luambano

DKT. KIRUSWA ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO CBT NA KUPONGEZA JUHUDI ZA RAIS DKT. SAMIA

Amani Ngoleligwe

VIONGOZI CBT WAKUTANA NA WAGENI KUTOKA UHOLANZI KUJADILI UONGEZAJI THAMANI ZAO LA KOROSHO

Amani Ngoleligwe